May 31, 2016

13267440_1166823470008599_165160329_n
Rapper Jay Moe amesema mashabiki wake watarajie ‘sound’ tofauti kwenye wimbo wake ujao uitwao Pesa ya Madafu.
Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, John Jackson aka JJ, rapper huyo mkongwe alisema video ya wimbo huo ilifanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Kwetu Studio.
“It’s a new different sound ya Jay Moe sio vile ambavyo watu wameexpect zamani, game imebadilika kwahiyo sikutaka kufanya hivi kwenye single yangu ya kwanza ndio maana tukaona tutoe kwanza Hili Game ambayo iko na ile feeling ya Jay Moe na hardcore rap. Sasa hivi tumeamua tuje tofauti zaidi kama ambayo zamani pia nilikuwa nafanya,” alisema rapper huyo.
Jay Moe ni miongoni mwa rappers wakongwe waliowahi kuwa na hits nyingi zikiwemo Bishoo, Cheza Kwa Step, Mvua na Jua, Story 3, Famous na zingine.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE