
Rapper mkongwe Joseph Mbilinyi aka Sugu amesema kuwa haoni faida ya bifu wanazoziendeleza wasanii wa Bongo.Sugu ambaye kwa sasa video yake ya ‘Freedom’ inafanya vizuri kwenye TV na redio, ameiambia Clouds TV, kupitia kipindi cha Clouds 360 kuwa haoni faida ya wasanii kuendekeza tofauti.
“Kuna vitu ambavyo mimi sivipendi sasa hivi , team nani team nani.Kwa sababu mtu akishafanikiwa akiwa pale top hatuhitaji wawe wawili au mmoja tunataka wawe wengi ili wakishafanikiwa watatoa ajira za kutosha,” alisema Sugu.
Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini aliongeza kuwa, “Mimi Sioni kama ina faida kwa sababu zinamfanya mmoja lazima apotee. Mimi nataka wote wanyanyuke.”
0 MAONI YAKO:
Post a Comment