Makongoro Oging’ enzi za uhai wake.
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging’ aliyefariki jana jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu aliugua kwa kipindi kifupi na alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yamemfika.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.
Ubalozini.blogspot.com tunatoa pole kwa Famili ya Marehemu na Kampuni ya Global kwa kuondikewa na kipenzi chao.
Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment