Ni masaa machache yamepita toka taarifa zinazoripotiwa kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF, kuripotiwa kuionya Yanga kutomtumia mchezaji Hassan Kessy hadi amalizane na Simba au Simba watoe barua ya kuridhia kumalizana na nyota huyo aliyejiunga na Yanga lakini mkataba wake unaisha mwezi June 31.
Ufafanuzi uliotolewa na CAF kupitia kwa afisa habari wake Junior Binyam ni kuwa Yanga wanaruhusiwa kumtumia mchezaji Hassan Kessy katika mchezo wa nane bora wa leo June 19 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria ila kama watakuwa wamekamilisha taratibu zote za usajili wa CAF, kama ambavyo inatakiwa.
Junior Binyam
“Kama
hakuna malalamiko kutoka katika klabu anayotoka ni jambo muhimu sana,
baada ya hapo ni kuangalia usajili wa CAF kama umefanyika kwa usahihi
kama kwenye mtandao au kawaida, ila suala la kuangalia kama mchezaji
amemalizana na klabu yake ni muhimu”
“Ninaamini wachezaji wao
watakuwa hawana tatizo kwa maana ya usajili wa CAF. Kwenye suala la
usajili katika klabu walizotoka, hili tunaweza kusubiri chama cha nchi
yenu (TFF) ndio waseme. Lakini hadi sasa, inaonekana wachezaji hao
wanaweza kutumika, hilo tuwaachie wao (Yanga).”
CHANZO: Salehjembe
0 MAONI YAKO:
Post a Comment