Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza majina ya
waamuzi watakaochezesha mashindano ya kombe la shirikisho Afrika kwa
hatua ya makundi yanayotarajiwa kutimua vumbi wiki ijayo.
Tanzania ikiwakilishwa na Yanga, inatarajiwa kucheza mchezo wake wa
kwanza wa hatua ya makundi Juni 19 na timu Mouloudia Olimpique Bejaia
kutoka Algeria, huku mchezo huo ukichezeshwa na mwamuzi kutoka nchini
Morocco [Bouchaib El Ahrach] akisaidiwa na washika vibendera, Redouane
Achik na Youssef Mabbrouk.
Aidha baada ya mchezo huo timu ya Yanga inatarajiwa kukutana na timu
ya TP Mazembe Juni 28 mchezo utakaochezwa uwanja mkuu wa taifa huku
mchezo huo ukiongozwa na mwamuzi, Janny Emiliano (Zambia) pamoja na
washika vibendera wake Jerson Emiliano (Angola) na Berhe O’michael
(Eritrea).
Timu nyingine zitakazocheza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ni
pamoja na MO Bejaia (Algeria) vs Esperance (Tunisia), Stade Malien
(Mali) vs FUS Rabat (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia) vs CF Mounana
(Gabon), TP Mazembe (DR Congo) vs Stade Gabesien (Tunisia), Ahli Tripoli
(Libya) vs Misr Makassa (Egypt), El Merreikh (Sudan) vs Kawkab
(Morocco), Young Africans (Tanzania) vs Sagrada Esperanca (Angola),
Mamelodi Sundowns (South Africa) vs Medeama (Ghana).
0 MAONI YAKO:
Post a Comment