Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF
Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na Mhe Jussa waliopowasili, kwenye
uwanja wa kimataifa Dulles Airport, Jijini Washington DC, siku ya
Jumamosi June 11, kwaajili ya ziara ya kikazi itakayochukua siku 14
nchini Marekani pamoja na Canada.
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amewasili
Washington DC amefuatana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa
Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa, na Katibu wake ambaye pia ni Mkuu wa
Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Issa Kheir Hussein.
Katika ziara hiyo, Maalim Seif na ujumbe wake watashiriki katika vikao
na mikutano maalum na pia kufanya mazungumzo na viongozi na maofisa wa
Serikali za Marekani na Canada, Wabunge wa nchi hizo, taasisi (think
tanks) zinazoshauri sera za mambo ya nje za nchi hizo, taasisi za fedha,
taasisi na jumuiya zinazohusika na masuala ya demokrasia na haki za
binadamu pamoja na vyombo vya habari.
Ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu, tarehe 13 Juni kwa kushiriki mkutano
ulioandaliwa na Centre for Strategic and International Studies (CSIS)
kujadili matokeo na matukio ya uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015
na nini unapaswa kuwa mwelekeo baada ya ubakaji wa demokrasia
uliofanywa.
Mbali na mikutano hiyo ya kikazi, Maalim Seif na ujumbe wake pia
watakutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchi jijini Washington
DC na vitongoji vyake.
Akizungumzia ziara hiyo wakati anaondoka akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere, mjini Dar es Salaam, Maalim Seif alisema: "Tumewaambia
Wazanzibari kuwa ni lazima tuidai haki yao ya maamuzi ya kidemokrasia
waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 kupitia kura zao .Tumewaambia tutaidai haki hiyo ndani ya Zanzibar, ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na katika jumuiya ya kimataifa. Ziara hii ni sehemu
muhimu ya kufanikisha malengo yetu katika uwanja wa kimataifa na
matunda yake yataonekana Inshallah".
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika mapokezi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment