Mitandao ya kijamii imekua ikirahisisha mfumo mzima wa upatikanaji wa
habari pia swala zima la sayansi na teknolojia. Pamoja na faida zake
hizo bado kuna madhara ambayo yanasababishwa na matumizi ya mitandao
hiyo ya kijamii. Hali ambayo imepeleka serikali ya Algeria kusitisha matumizi ya mitandao ya kijamii kwa sasa.
Hii imetokana na kuwepo kwa udanganyifu wakati wa mitihani ambapo
wanafunzi walibainika kutumia mitandao ya kijamii kuvujisha mitihani.
Hivyo serikali imewalazimu kutotumia mitandao ya kijamii kwa kipindi
hichi ambacho wanafunzi wa sekondari wanafanya mitihani ya kuhitimu ili
kujiunga na elimu ya juu.
Uvujishaji wa mitihani kupitia mitandao ya kijamii umekuwa tatizo kwa
muda sasa nchini humo. Serikali inaamini kwa kufanya hivyo itasaidia
kupunguza matukio kama hayo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment