Ushirika
wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT)umeiomba
serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat
Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na
kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Mwenyekiti
wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake
katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga amesema,kauli hizo zinaweza
kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na
kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Askofu
Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na
kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa
na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti
huyo wa ppft amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa
Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwaa la
kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na
iliyopo madarakani.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment