Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada
ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema
wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao
kujiunga na chuo hicho.
Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha
kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.
“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.
“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la
kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya
kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom,
hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.
“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”
Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais
John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.
Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua
kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.
“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote
waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na
wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki
mahakama,” alisema Lusako.
Udom yazungumza
Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote
walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la
tatu.
“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa
kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya
moja kwa moja,” alisema.
Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada
kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda
mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.
“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna
tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi
Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.
My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?
0 MAONI YAKO:
Post a Comment