MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati,
Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu
ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine
wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo
ambalo si kweli.
Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond
ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa
baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti akisema hana mpango wa
kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake, Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.
Wema
alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28 kama
ilivyo kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku
akisisitiza amempa likizo Diamond.
Staa huyo asiyekaukiwa na
matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna
wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye
haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni
mawazo ya muda mrefu.
“Kwanza naomba watu
wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni
shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua
kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi,” alisema
Wema.
Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa
lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku
zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya
kisiasa tu.
“Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu
ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine
yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka .
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka .
Wakati Diamond akisema hayo,
baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha
ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”
Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment