June 07, 2016

8
Muigizaji maarufu wa Marekani Will Smith na Bondia wa Uingereza Lennox Lewis ni miongoni mwa watu nane walioteuliwa kubeba jeneza la bondia maarufu wa zamani wa Marekani aliyefariki dunia Muhammad Ali katika mazishi yake siku ya Ijumaa.
Pamoja na hao wawili, wengine watakaobeba jeneza la Ali ni pamoja na binamu wa Ali, John Grady na Jan Wadell, Ibn Ali, aliyekuwa shemeji yake Komawi Ali na rafiki wa familia John Ramsey
Maelfu ya watu wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya bondia huyo katika mji wa Louisville siku ya ijumaa.
Rais wa Uturuki na Mfalme wa Jordan ni miongoni mwa watu watakaozungumza katika mazishi hayo, wakati Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton yeye atazungumzia umashuhuru wa Muhammad Ali.
Pamoja na hao wote, pia mke wa Muhhamad Ali, Lonniel Ali, mtoto wake Maryum Ali na mchekeshaji Bill Crystal watazungumza wakati wa mazishi ya Ali aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi wiki jana akiwa na umri wa miaka 74.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE