July 06, 2016

 

Baraza la vijana la Chadema mkoa wa Iringa chini ya uongozi wa BAVICHA mkoa iringa na viongozi wote wa baraza kwa ngazi zote za wilaya, majimbo, kata, matawi na misingi tumekubaliana na kuunga mkono kwa
asilimia mia moja tamko la baraza la vijana Taifa lililotolewa na makamu mwkt ndugu Patrick Sosopi la Tarehe 02/07/2016 la kukutana Dodoma Tarehe 23/07/2016 ili kulisaidia jeshi la polisi kuwataka wenzetu
CCM kutii sheria bila shuruti.
Na kwa mantiki hiyo tunatangaza rasmi kuanzia leo tarehe 06-15/07/2016 zoezi la kuandikisha vijana kwa ngazi zote za uongozi litafanyika mkoa wa Iringa na kwakuwa vijana wengi wamekuwa wakitupigia simu
kuonyesha utayari wao basi sasa tunawaalika rasmi kujiandikisha. 

Ndugu, Wanahabari mtakumbuka mwkt wa kamati ya siasa ya CCM Iringa mjini ndugu Kiponza aliwaita na kuzungumza nanyi, pamoja na mambo mengine alieleza kile alichoita kuwa ndoto za bavicha kuzuia mkutano wa CCM haziwezekani.sisi tunawaambia wenzetu waache kuweweseka na wasubiri tarehe 23 ili wajue jinsi nguvu ya kisia navyoweza kusimamia amri ya jeshi la police pamoja rais wao ya kuzuia shughuli za kisiasa mpaka 2020 . Pia watambue kuwa kupingana na bavicha ni sawa na kupingana na agizo la mh. Rais tena aliyetokana na chama Chao, jambo ambalo si heshima kwa kiongozi wetu wa nchi. Pia niwakumbushe ccm sisi bavicha mkoa wa Iringa hatuendi Dodoma kufanya vurugu na uchochezi kama wanavyosema wao bali tunaenda kuwasaidia police kuzuia mkusanyiko harama wa ccm 

Ndugu Wanahabari, Naomba ieleweke kuwa ninyi wenyewe ni mashahidi wa Tamko lilitolewa na mkuu wetu wa nchi ambalo lilikwenda sambamba na tamko la jeshi la polisi kuvitaka vyama vyote vya siasa na wanasiasa wasijihusishe na shughuli za kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuwapa fursa viongozi waliochaguliwa kutekeleza ilani na ahadi zao kwa wananchi. Sasa sisi tunajiuliza kwanini CCM wanataka kukaidi agizo hili
wakati vyama vingine vimekubali na kutii? Havana, ni lazima twende Dodoma tukawaambie CCM wajifunze kutii maagizo ya vyombo vya dola na viongozi wa nchi. KWANINI TUNAKWENDA DODOMA?
Ndugu Wanahabari tunakwenda Dodoma
kwakuwa,
 
01. Mpaka sasa si rais wala jeshi la polisi
aliyetengua kauli au tamko la kuzuia
shughuli za kisiasa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE