Akiongea na Bongo5, Dayna amesema kuwa kwa sasa ideas nyingi anazokuwa nazo zinahitaji sana wasanii wa kiume pekee.
“Siwezi kusema kuwa nawatenga wasanii wenzangu wa kike kufanya nao kazi, kila kitu kina wakati wake. Nitafanya nao kazi pale nitakapoona inahitajika nifanye nao kazi. Nashindwa kufanya nao kwa sasa kwa sababu idea nyingi ninazokuwa nazo zinahitaji wasanii wa kiume pekee,” amesema Dayna.
“Lakini nashukuru angalau nilishawahi kufanya kazi na Misoji Nkwabi aliyekuwa mshindi wa BSS,” ameongeza.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment