![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfH3fOD11eDoVUbrb8jDgGA3MjuNlhLXfyGdFcEeBKZCU5unCmmAQGE51bBUDIbmFHeU2af3SnLoxMk41xKy9iH__NDBymXfu7QK2z4f8kstgSwh4euGzMaU_9i6VXJznqCRZdgXjaeU4/s400/1.jpg)
Mtunzi: Enea Faidy
..Mwalimu
John alipelekwa makuburini kwaajili ya mazishi ingawa yeye alijiona
yuko hai. Dorice alikuwa njiani baada ya kutoroka shulen, na alipofika
kwenye kijito kidogo alishtushwa na kishindo kikali.
Eddy alifikia hatua ya Mwisho kutaka kufanya mapenzi na Doreen lakini kabla ya kufanya hivyo aliachia yowe Kali.
SONGA NAYO UJUE KILICHOJIRI....
....VIJANA
wanne wenye nguvu walinyanyua jeneza alililokuwamo Mwalimu John kisha
taratibu walipiga hatua kuelekea kwenye nyumba yenye pembe NNE na kina
kirefu kiasi aliyotengenezewa mwalimu John.
Sauti
za vilio zilizidi kutia simanzi katika eneo lile LA makaburini. Nyimbo
za huzuni zilitawala eneo hili huku kila mmoja akisikitika moyoni mwake.
Ndani ya jeneza hilo mwalimu John alikuwa akihangaika sana kuwaita vijana wale ili wasimzike lakini katu hakusikika.
Alizidi
kupiga kelele za kuomba msaada lakini ikabaki kuwa kazi bure. Sauti
iliyojaa huzuni kuu ya mkewe Monalisa ilizidi kupenya vyema masikioni
mwake, hali hii ilizidi kumtia simanzi mwalimu huyo ambaye sasa alikuwa
amekata tamaa ya kuishi tena.
"Daah
Doreen hafai" alijisemea mwalimu John huku machozi yakimtiririka kwa
kasi kwani bado alikuwa haamini kama kweli anazikwa akiwa mzima.Vijana
wale walilishusha jeneza lile lenye mapambo ya kupendeza ndani ya kaburi
kisha wakatulia kidogo ili mchungaji atupie neno La mwisho.
Mchungaji
alichukua udongo kidogo na kusogelea vyema kwenye shimo alilowekwa
mwalimu John."Uliumbwa kwa mavumbi hakika utarudi mavumbini, Bwana
alitoa Bwana ametwaa jina La Bwana lihimidiwe... " Mchungaji aliyasema
maneno hayo kwa huzuni kisha akaumwaga kaburini udongo ule aliokuwa
ameushika mkononi.
Mwalimu
John aliyasikia vyema maneno hayo yaliyouchoma moyo wake kama mkuki
wenye sumu. Hakika mwalimu John alikiri kuwa kweli duniani kuna watu na
viatu, Doreen alikuwa kiatu chakavu kisichofaa kuvaliwa hata na kichaa.
Vijana
walishika vyema sepetu zao ili waanze kutupa udongo kaburini na kumzika
mwalimu John lakini kabla hawajaanza kutupa udongo, kilizuka kimbunga
kikali cha ghafla kilichofanya watu wapoteane. Jeneza likafunuka ghafla
mwalimu John akainuka kutoka kwenye jeneza.
Itaendelea wiki ijayo
0 MAONI YAKO:
Post a Comment