July 03, 2016

MAHADHI: NIPO TAYARI KWENDA MAZEMBE
Winga wa Yanga Juma Mahadhi amesema yupo tayari kutimkia TP Mazembe endapo timu hiyo itamuhitaji  lakini amewataka watoto hao wa tajiri Moise Katumbi, wakutane na uongozi wa timu yake ya Yanga.
Mahadhi ameiambia Goal, siku zote amekuwa akitamani kupata mafanikio kupitia kipaji chake cha soka hivyo hawezi kukataa ofa hiyo kama Mazembe nikweli watakuwa wanamuhitaji ajiunge nayo kutokana na vutiwa na kiwango chake.
“Nimefurahi kuona timu kubwa kama TP Mazembe inanihitaji,  kwasababu ni moja ya nanfasi nilizokuwa nikizitafuta siku nyingi kutokana na ukumbwa wa timu hiyo nitaweza kuonekana zaidi duniani lakini nivyema hao Mazembe wakakutana na uongozi wa Yanga kwasababu mimi ni mali yao na ndiyo kwanza nimejiunga nao sina hata mwezi mmoja,”amesema Mahadhi.
Mazembe walionekana kuvutiwa na kiwango cha winga huyo ingawa ilikuwa ndiyo mechi yake ya kwanza tangu atue Yanga lakini alionyesha uwezo mkubwa na kuwasubua sana mabeki wa Mazembe ambao walilazimika kumuumiza dakika ya 65 na kutolewa nje.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE