MACHAKU MEDIA
facebook tweeter google linked in you tube rss

MACHAKU MEDIA TUNAKUKARIBISHA HAPA KWA MATANGAZO.

TUMEKUKUTANISHA NA GAVAO LODGE.

KAMA UNAPENDA MOUVE HII NDIYO SEHEMU YAKO.

First slide Next

July 02, 2016

  • 11:16 PM
  • Machaku
  • No comments

Video: Tamko la BAVICHA kuhusu kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM Julai 23

12
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitoa zuio la mikutano ya siasa ya wazi na ya ndani nchini kote, hata hivyo CCM imepanga kufanya Mkutano Mkuu tarehe 23 Julai mwaka huu mjini Dodoma.

Kwenye mkutano huo, Dk. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM atakabidhi mamlaka hayo kwa Dk. John Magufuli ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa chama hicho.

Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limepanga kuzuia mkutano huo kwa madai ya kulisaidia Jeshi la Polisi kusimamia agizo lake kwa vyama vya siasa nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Slaam viongozi wa Bavicha walisema, hatua hiyo ni katika kuhakikisha wanalisaidia jeshi kutekeleza amri iliyotolewa na Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020.

“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokwenda Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM.  Kwa sababau Jeshi la Polisi limezuia mikutano yote ya siasa kwa sasa.

“Pia ni katika kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli kwamba, hakuna mikutano ya vyama vya siasa mpaka mwaka 2020. Huu ndio msiamamo wa baraza.

“Mikutano yetu sisi kama Chadema tunazuiwa lakini CCM wanafanya. Mahafari ya chama cha mapinduzi yanafanyika. Ni jana CHASO (Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema) Morogoro tumezuiwa lakini UVCCM (Umoja wa Vijana wa CCM) Mkoa wa Morogogo wamefanya na picha zipo. Hii sio haki, kama mbwai na iwe mbwai,” alisema Patrick ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo.

George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya alisema “… ni kwamba, huko mikoani vijana wameshajipanga. Wana ari kubwa ya kwenda Dodoma.

“Tumeamua kufikia hatua hii kwa sababu tumekuwa tunaona hakuna haki katika nchi hii. Kuna mahafali yanafanyika vyuo vikuu, wenzetu CCM wanaruhusiwa sisi Chadema tunakatazwa.Vijana wa Chadema wamekuwa wakikamatwa bila sababu za msingi,” alisema Tito.



Tazama Video hapa chini
                 

                  
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
← Newer Post Older Post → Home

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • ALICHOANDIKA DIAMOND BAADA YA MSIBA WA BABA YAKE WEMA SEPETU
  • TAZAMA DJ FETTY AKITOA BURUDANI NDANI YA AMBASSADOR LOUNGE AKISINDIKIZWA NA MULLY B NA DJ ZERO
                                                                         Dj Fetty                                                   ...

WADAU

BLOG ZINGINE

  • MALUNDE 1 BLOG
    HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 12,2025 - Magazeti Magazeti
    1 hour ago
  • MwanaHALISI Online
    Jenister Mhagama atimiza ndoto za Rais Samia utalii tiba - WAZIRI wa Afya, Jenista Mhagama amesema ili kufikia ndoto kamili za Tanzania kuwa kitovu...
    5 hours ago
  • Bongo Blogs - Blog ya Taifa
    Majina ya Blog Zinazoanzia na Herufi ya V - *1. VOA Sauti ya America * www.voaswahili.com *2. Vijimambo* lukemusicfactory.blogspot.com
    4 months ago
  • Mbeya City Council FC
    37岁姚笛沉寂六年高调复出,短发造型撞款马伊琍,这次真的没有输 - 37岁姚笛沉寂六年高调复出,短发造型撞款马伊琍,这次真的没有输近期姚笛为杂志拍摄的一组大片曝光后,将这么在影视圈沉寂六年的大眼美人又推上了新闻热点。姚笛受当年事情的影响,在红极一时的大女主时期被雪藏。...
    5 years ago
  • UBUYU
    Taarifa Ya Serikali Kuhusu Mwenendo Wa Hali Ya Uchumi Na Utekelezaji Wa Bajeti Ya Serikali Kwa Mwaka 2017/18 - *­­­* *UTANGULIZI* Nashukuru sana kupata fursa nyingine ya kuzungumza nanyi leo tunapokaribia mwisho wa mwaka 2017. Lengo la Serikali ni kuwapatia Watanza...
    7 years ago
  • Hassbaby's (Mapacha)
    Amber Lulu Ft Country Boy - Watakoma |Download Mp3 - Amber Lulu Ft Country Boy - Watakoma |Download Mp3
    8 years ago
  • Dr Isaac Maro
    Comment Déverrouiller (“désimlocker”) El IPhone Assistance - Tout d’abord, j’ai besoin de corriger un erreur concernant le produit Gevey ultra S SIMA una dernière weblog j’ai ditgene que writer numéro d’urgent 112 ...
    8 years ago
Copyright © MACHAKU MEDIA
DESIGN BY DISMAS TEN | O713216125