Muonekano wa jiji la Kampala nchini Uganda
RFI/Victor Abuso
Takribani watu 20 wamepoteza
maisha leo Jumapili katika ajali ya barabarani kwenye barabara kuu nje
ya mji mkuu wa Uganda, Kampala na wengine kadhaa wamejeruhiwa,wengine
wako katika hali mbaya polisi imesema.
Msemaji wa polisi Phillip Mukasa
ameithibitishia AFP taarifa za ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi
wamepelekwa hospitalini kutoka na majeraha makubwa waliyopata.
Magari matano yamehusika katika ajali hiyo katika barabara kuu ya
Kampala-Masaka wakati gari binafsi lilipokuwa likijaribu kuyapita
magari mengi katika njia yenye magari mengi umbali wa kilometa 150
Kusini Magharibi mwa mji mkuu Kampala.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment