Zari
Hassan maarufu kama Zari the Bossylady kutoka Uganda, na mzazi mwenza
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ambaye ni mwanamuziki wa kizazi
kipya kutoka hapa nchini, Amezuiliwa kuendesha event yake ya ‘Zari All
White Party’ hapa nchini Tanzania na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)
kwa kile kinachosemekana kwamba hakutimiza masharti aliyowekewa kabla ya
kufanya event hiyo mara ya mwisho kufanyika hapa Dar es salaam.
Zari alianza kufanya matangazo ya event
yake kabla ya hajakamilisha taratibu zote za BASATA mnamo mwaka 2014, na
kwa kosa hilo alipewa faini ya kiasi cha fedha TZS 460,000/- na
kuzuiliwa kufanya event hiyo hapa nchini mpaka atakaporuhusiwa, na hiyo
ni endapo atafata kanuni na taratibu zote alizowekewa na Baraza la
Sanaa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment