August 08, 2016

Aziz
Na Baraka Mbolembole

Shaaban Kisiga, Hassan Dilunga na sasa Ruvu Shooting imefanikiwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja kiungo ‘fundi’ Jabir Aziz ‘Stima.’
Nahodha huyo wa zamani wa Azam FC ambaye alipata pia kuzichezea Ashanti United na Simba SC miaka ya nyuma amejiunga na Shooting ya Mlandizi, Pwani akitokea Mwadui FC ya Shinyanga.
“Ni kweli nimesaini Shooting mkataba wa mwaka mmoja,” anasema, Stima mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambaye alifunga goli pekee la Stars katika kichapo cha 5-1 kutoka kwa Brazil, Juni, 2010 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akiwa nahodha wa Mwadui FC, Stima alicheza game 27 za VPL msimu uliopita na nyingine 3 katika FA Cup. Shooting iliyorejea VPL msimu huu sasa itakuwa na viungo hao watatu wachezesha timu wenye uwezo wa hali ya juu uwanjani.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE