Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametoa amri ya kufutwa kazi mawaziri wote wa aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Vikosi
vinavyowatii viongozi hao wawili vilihusika katika mapigano mapya
mnamo mwezi Juni na kuwawacha mamia wakiwa wamefariki na maelfu bila
makao.Baada ya kukubaliana kuhusu kusitisha vita,bw Machar alienda mafichoni na mahala pake pakachukuliwa na Taban Deng ambaye alikuwa waziri wa madini,hatua ambayo Machar anasema ni kinyume cha sheria.
Mawaziri ambao wamefutwa kazi ni.
1. Alfred Ladu Gore, waziri wa maswala ya ndani
2. Duk Duop Bichok, Waziri wa mafuta
3. Dr Peter Adwok Nyaba, Waziri wa Elimu ya juu ,Sayansi na Teknolojia
4. Peter Marcello Nasir Jelenge, Waziri wa Leba,Huduma ya uma
5. Mary Alfonse Lodira, Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya mijini.
6. Mabior Garang de Mabior, Waziri wa Maji na kilimo cha Unyunyizaji.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment