August 24, 2016



MKE wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Elisaria Msuya (41) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya dada wa wa bilionea huyo, Aneth Msuya.

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi, Margareth Bankika.

Akisoma mashtaka hayo, Lukondo alidai mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa maeneo ya Sakina kwa Iddi, jijini Arusha anadaiwa Mei 25, mwaka huu katika maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam alimuua Aneth Elisaria Msuya.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji, mbapo Jamhuri ilidai upelelezi haujakamilika na kuomba kesi hiyo ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Bankika, alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alirudishwa rumande.

Habari zilizopatikana baada ya tukio hilo zilidai kwamba, marehemu Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Mei 25, mwaka huu Dar es Salaam.

Mauaji hayo yalitokea nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni ambako inaelezwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Marehemu Erasto Msuya, aliyekuwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliuawa kwa kufyatuliwa risasi Julai 7, mwaka 2013 katika eneo la Mijohoroni,  kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akiwa ameitika wito wa kwenda kununua madini ya Tanzanite baada ya kupigiwa simu na vijana wawili  waliomtaka wakutane maeneo hayo.

Inaelezwa kuwa alifika katika eneo hilo akiwa na gari lake aina ya Range Rover T 800 CKF na kuwakuta vijana hao wakimsubiri, baada ya kuteremka Msuya alielekea kumsalimia mmoja wa vijana hao.

Hata hivyo kabla hajamfikia kijana huyo aliitoa bunduki ya SMG namba KJ 10520 aliyokuwa ameificha kwenye koti na kumfyatulia risasi takribani 22 mwilini.

Related Posts:

  • Watumishi hewa Dar es salaam wafikia 209, Makonda aamua kufanya hivi Wakati watumishi hewa kwa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongezeka na kufikia 209, wakuu wa idara za mkoa na manispaa wametia saini na kula kiapo kuwabaini bila kuficha ukweli. Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa huo, Paul Mako… Read More
  • Rais wa Burundi amefariki DuniaRais wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki akitibiwa nchini Ubelgiji. Kanali Bagaza amekuwa akitibiwa kwa muda katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels. "Imethibitishwa, rais wa zamani Jean Bap… Read More
  • Sim yamponza Justin Bieber   Mwanamuziki Justin Bieber ameshtakiwa kwa dola milioni 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu. Nyota huyo ametuhumiwa kuivunja simu ya Robert Earl Morgan baada ya kujaribu kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akiny… Read More
  • Serikali yasitisha wimbo na Video ya Chura ya Snura mpaka ..... Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kuisitisha video na wimbo wa Snura, Chura kuchezwa kwenye redio na TV. Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zaw… Read More
  • Mtoto wa miaka 10 agundua udhaifu Instagram Mvulana wa umri wa miaka 10 nchini Finland ameshangaza wengi baada ya kugundua udhaifu katika mtandao wa kijamii wa Instagram. Mvulana huyo kwa jina Jani ametunukiwa $10,000 (£7,000) baada ya kugundua udhaifu huo ulio… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE