Ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Rio2016
2.50am:Kikosi cha wanariadha wa Olimpiki kutoka Australia ndio hao wanapita mbele ya mashabiki wanaowapongeza
Wanariadha wa Australia
2.45am:Tayari mataifa yanayoshiriki yameanza kuingia katika uwanja wa Mariccana huku shangwe na nderemo zikipamba hewani.20.30am:Fataki zilizorushwa katika ufunguzi wa michezo ya Rio2016
Fataki za aina mbali mabli zilirushwa katika ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki nchini Brazil
2.15am: Usalama uliimarishwa nje ya ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo katika eneo la Barra huku vikosi vya kijeshi vikisambazwa katika kila eneo la mita 25.msongamno wa magari sio mkubwa usiku huu.Inaonekana kwamba wakaazi wa Rio wanafuatilia ufunguzi katika runinga zao majumbani mwao!
Usalama umeimarishwa katika ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo
2.10am:Wakati huohuo takriban waandamanji 200 walipiga kambi katika ukumbi wa saens Pena nchini Brazil ili kupinga michezo hiyo,ikiwa ni mita chache kutoka eneo linalofanyiwa sherehe za ufunguzi wa michezo.
Waandamanaji mjini Rio
Maandamano hayo yalioanza mwendo wa saa nane siku ya
ijumaa yalikamilika katika ukumbi huo mwendo wa saa kumi na kuelekea
katika uwanja wa Marrica.kulikuwa na ripoti za ghasia katika barabara
inayoelekea katika uwanja huo lakini baadaye zilisitishwa na
muandamanaji mmoja alijeruhiwa.2.05am:Takriban mataifa 200 yanashiriki katika michezo hii.Sherehe hizo zimeanza kwa kurushwa kwa fataki huku mashabiki waliotoka katika seshemu mbali mbali za ulimwengu wakifurahia.
Mashabiki wa Brazil waliojaa katika uwanja wa Mariccana
2.00am: Ni mbwembwe na furaha za
aina mbali mbali katika uwanja wa Mariccana ambapo sherehe za ufunguzi
wa michezo ya Olimpiki zimeanza.Sherehe za Ufunguzi wa michezo ya Rio2016
Chanzo:BBC
0 MAONI YAKO:
Post a Comment