August 04, 2016

.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa bongo wakongwe kuanzisha label mbalimbali ambazo zinakuwa zikiwasimamia kazi wasanii wadogo kwa lengo la kufanya biashara lakini kwa upande wa Ben Pol amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa uwezo wake haujafikia katika kumsimamia
msanii kwa kila jambo
Bali anaweza kumsaidia msanii katika baadhi ya mambo kama kumlipia wimbo na kumpa connection msanii pamoja na kumpa njia mbalimbali za kupita ili afikie malengo yake lakini hana uwezo wa kumsimamia msanii kwa kila kitu.

Ben Pol anasema kwa uwezo wake alionao sasa anaweza tu kumlipa wimbo, kumasaidia connection na namna nzuri ya kutangaza kazi zake ila kufanya kila kitu kwa msanii uwezo huo hana.

"Mimi niwe mkweli tu, siwezi kusema namsaidia msanii kwa kila jambo uwezo wangu mimi kwa sasa labda nimlipiwe wimbo, nimsaidie connection na kumpa njia mbalimbali za kutangaza ngoma zake, lakini kusema nimfanyie msanii kila kitu sijui kuanzia wimbo, na kila kitu mpaka video hapana uwezo huo kwa sasa sina" alisema Ben Pol

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE