Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki
TUNDU Lissu Mbunge wa Singida Mashariki ametiwa mbaroni na jeshi la Polisi Mkoani Sindiga mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara, anaandika mwandishi wetu.
Taarifa zinasema kuwa Lissu alikamatwa mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo katika Jimbo lake eneo la Ikungi mkoani humo.Chanzo cha habari hizi kinaeleza kuwa Lissu alikamatwa na Ofisa Mkuu wa Makosa ya Jinai wa jeahi hilo aliyejitambulisha kama Babu Mollel kwa maelekezo ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Singida na kwamba maelekezo hayo yanatoka Jijini Dar es Salaam
Taarifa zinasema kuwa Lissu usiku huu anaweza kusafirishwa hadi Jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinasema kuwa Lissu amekatwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi Jana Tarehe 2 Agosti mara baada ya kutoka katika mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akizungumza na wafuasi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo Chadema.
Mtandao huu utakujuza kila kinachoendelea.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment