August 25, 2016

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini vimemshauri Rais John Pombe Magufuli kuvifuta vyama vya upinzani kama anaona vinamsumbua anapofanya mambo yake.


Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia ambapo amesema kuwa kama Rais Magufuli anaona vyama vya upinzania vinamkera na kumkwamisha anapotaka kufanya jambo basi serikali yake ipelekea mswada kwa hati ya dharura bungeni ili kufanya mabadiliko katika sheria ya vyama vya siasa na kuvifuta vyote.



Mbatia amesema kuwa jambo hilo amelitafakari na kuwashirikisha viongozi wenzake na huenda ikasaidia kwa sababu Rais Magufuli anaonekana kutaka kuongoza kwa kutumia akili yake na hataki kukosolewa na mtu yeyote wala chama chochote.



Katika hatua nyingine, viongozi wa vyama vya upinzani wameitikia wito wa viongozi wa dini uliowataka kurudi bungeni na wameahidi kuwa watajadiliana na wanaamini watafikia muafaka na kurudi bungeni katika mkutano ujao mwezi wa tisa.



Tazama video hapo chini


SeeBait
                

Related Posts:

  • CCM wamjibu Maalim Seif Muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wam… Read More
  • Al-Shabab wako 'huru' kushiriki soka SomaliaWapiganaji wa Alshabaab Mkuu wa shirikisho la soka nchini Somalia amesema kuwa kundi la wapiganaji wa al-Shabab liko huru kushiriki katika ligi kuu ya soka nchini humo. Abdiqani Said Arab amemuambiwa mwandishi wa BBC jijini N… Read More
  • Magazeti ya leo january12 ya 2016 yanasema hivi Karibu mpenzi mwana familia wa ubalozini.blogspot.com . Leo ikiwa ni jumanne ya January 12 ,2016 ikiwa ni siku ya mapinduzi ya Zanzibar, tumekukusanyia vichwa vya habari za magazetini kama yalivyotufikia. … Read More
  • Mufti wa Tanzania ampa baraka Mbwana Samatta Jana tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Ndg. Mbwana Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Mufti Mkuu mbali na kumpa… Read More
  • CUF yapinga marudio ya uchaguzi Zanzibar Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar. Chama hicho kupitia taarifa kwa wanahabari kimesema hakuna “hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi kurudiwa&#… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE