September 30, 2016

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewataka wanachama wa chama hicho na watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa za utafiti za wa taasisi ya Twaweza, anaandika Pendo Omary.


Tamko la Mbowe limekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Twaweza, kutangaza matokeo ya utafiti wake uliopewa jina la ‘Demokrasia, udikteta na maandamano.’

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema Twaweza ni wapiga zumari wanaochaguliwa wimbo na watawala wa kiimla ili kujaribu kufunika aibu inayolikabili taifa letu kwa sasa.

“Hatua zinazochukuliwa na Rais John Magufuli zimeporomosha uchumi wa nchi yetu kwa kiasi cha kutisha. Mapato ya wananchi yameanguka. Uwekezaji wa ndani na nje ya nchi umepungua. Ajira zimepungua kwa kiasi kikubwa na umasikini umeongezeka,” amesema Mbowe.

Ripoti ya utafiti wa Twaweza iliyokusanywa kutokana na wahojiwa 1,602 kati ya tarehe 23 na 29 Agosti, mwaka huu kwa njia ya simu Tanzania Bara, imesema kwamba watu 6 kati ya 10 wamepinga madai kuwa nchi ya Tanzania inaongozwa kidikteta.

Hata hivyo Mbowe amesisitiza kuwa, kwa sasa mifumo ya kikatiba na kisheria ya uendeshaji wa nchi na serikali imevurugwa kwa kiasi ambacho nchi inaendeshwa kwa amri na vitisho vya mtu mmoja.
Aidha, Mbowe amesema Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chadema inatambua mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi- CUF, unaomhusisha aliyekuwa Profesa Ibrahim Lipumba unachochewa na Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Jaji Mutungi anaivuruga CUF kwa kujaribu kumrudisha madarakani Prof. Lipumba, ambaye alijiuzulu madarakani katika mazingira yanayoashiria kununuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kusaliti vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Chadema hatumtambui Prof. Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF Taifa au Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, tunamtambua kama adui wa demokrasia na msaliti wa harakati za kudai haki katika nchi yetu,” amesema Mbowe.

Mbowe ameongeza kuwa, Jaji Mutungi pia ni adui wa demokrasia ya vyama vingi na kwamba Chadema haitampa ushirikiano wowote isipokuwa ule tu unaolazimishwa na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Kuhusu uzinduzi wa oparesheni ya Ukuta iliyotarajiwa kuzinduliwa tarehe 1 Oktoba, mwaka huu, Mbowe amesema mikutano na maandamano hayo yatafanyika kwa siku na tarehe itakayopangwa hapo baadaye kwa kuzngatia hali halisi ya kisasa itakayokuwepo nchini.

Related Posts:

  • KANUMBA FILM, KUSHUSHA KIPYA   Kampuni ya filamu za Kibongo Kanumba The Great Films imeingia mzigoni kuandaa filamu mpya iitwayo WONDER GIRL ikiwashirikisha waigizaji mahiri wa tasnia hiyo.   … Read More
  • NAY WA MITEGO,MADAM RITA SASA DAMDAM   Mwanamuziki wa Hiphop Bongo,Emanuel Elibarik‘Nay wa Mitego’na Mkurugenzi wa Benchmark Production Rita Paulsen‘Madam Rita hawana tofauti, baada ya kupiga picha ya pamoja katika uzinduzi wa vid… Read More
  • FOOLISH AGE YA LULU. TIKETI KUUZWA MLANGONI     Tiketi za uzinduzi wa LULU Bado zinapatikana na Zitauzwa Mlangoni Kwa Gharama za shilingi Elfu 30 tu. UZINDUZI UNAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY KUANZIA SAA MOJA JIONI. usikose wahi sasa … Read More
  • LULU ATAJA SEHEMU ZINAZOPATIKANA TIKETI ZA UZINDUZI WA FOOLISH AGE Staa wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael‘Lulu’ametangaza rasmi sehemu zinzopatikana tiketi za uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age inayotajiwa kuzinduliwa August 30,Mlimani City,Dar. Lulu ameposti tiketi hizo kupit… Read More
  • CRAZY GK NA BARAKA AU LAANA Baada ya kupotea kwenye muziki kwa muda mrefu sana Crazy Gk amerudi kwa kishindo na kuzindua wimbo wake mpya huku akisindikizwa na timu ya East Coast Team. Sababu kubwa iliyopelekea King Crazy Gk kupotea kwenye game… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE