September 03, 2016

 
Wasanii wa Fiesta2016 na Wafanyakazi wa CloudsMediaGroup wakabidhiwa watoto; Semina ya Fursa2016 imefanya tukio la kipekee mjini Shinyaga baada ya kuwachukua watoto wenye Ulemavu kutoka katika kituo cha Buhangija na kuwakabidhi kwa wasanii wa #Fiesta2016 ambao wamekubali kuchukua jukumu la kuwalea watoto hao ( Kila mmoja amekabidhiwa mtoto mmoja).

 
Dyna Nyange ni kati ya Mabinti waliopata Ujauzito katika Umri Mdogo; Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Agape Knowledge Open School katika kampeni ya #Kipepeo Mkoani Shinyaga, Dyna amesisitiza kwamba yeye hajutii kitendo hicho tena anashukuru Mungu kwani kupata mtoto ni bahati ambayo kuna watu wengi wanaikosa.

" Siwapongezi kwa kupata watoto katika umri mdogo; lakini hampaswi kujutia na kuona kwamba ndoto zenu zimefikia mwisho. Jambo la msingi ni kutokukata tamaa , na mnatakiwa kusonga mbele katika maisha yenu " Alisema Dyna.

Dyna amewapongeza Wanafunzi hao kwa uamuzi wao wa kurudi shule na amewasisitiza 'kukomaa' na masomo.

 
 Darasa amesema kwamba anaishukuru sana #Fursa2016 kwa kuja na wazo la kuwasaidia watoto. Darasa alisisitiza kwamba yeye ni alilelewa katika mazingira magumu sana na kwa muda mrefu alikosa 'love' ya familia na hivyo anafahamu Uchungu wa kukosa upendo huo. Darasa amempokea mtoto Elizabeth na kuahidi kwamba atahakikisha anamlea kama ndugu yake wa damu.

 
 Msanii na Mzungumzaji katika #Fursa2016 , @nikkwapili ameahidi kumlea mtoto Steven ikiwa ni pamoja na kusimamia Elimu yake. Nikki wa Pili ameahidi kwamba kwa uwezo wa MUNGU atasimama mpaka Steven apate 'Degree' kama yeye
 
 @chemical_tz na Prisca; ni kama walijipanga Chemical avae nguo ya njano na Prisca kofia ya njano.
Chemical aliamua kuazisha urafiki wa dhati na Prisca na ameahidi kuwa naye karibu siku zote.


 
                               

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE