Afisi ya chama cha Republican iliopigwa bomu katika kaunti ya Orange nchini Marekani
Afisi moja ya chama
cha Republican katika jimbo la North Carolina imeharibiwa na moto huku
jengo lililo karibu yake likipakwa rangi ya nembo inayopinga chama cha
Republican,mamlaka imesema.
Chupa iliojazwa mafuta yanayoweza
kushika moto ilirushwa katika dirisha la makao makuu ya chama cha
Republican kaunti ya Orange,chama hicho kimesema.
Mkurugenzi wa
chama cha Republican, Dallas Woodhouse alisema kuwa hakuna mtu
aliyejeruhiwa,na kwamba tahadhari ya kiusalama imetumwa katika afisi
nyengine za chama hicho.
''Wanachama wa Nazi walio katika chama cha Republican ni sharti waondoke mjini''.
Mgombea
wa Democrat Hillary Clinton ameandika katika mtandao wake wa Twitter
kwamba shambulio hilo ni ''la kutisha na halitakubalika''.
Lakini Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alionekana
akiwalaumu wafuasi wa chama cha Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho.
''Wanyama
wanaomwakilisha Hillary Clinton huko North Carolina walirusha bomu
katika ofisi yetu ya kaunti ya Ornge kwa sababu tunashinda'',alisema
katika mtandao wake wa Twitter.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment