Afisa wa zamani wa ngazi ya juu
nchini China, aliyepatikana ameficha dola za Kimarekani 30 milioni
nyumbani mwake, amehukumiwa kunyongwa.
Hukumu hiyo hata hivyo imeahirishwa.Wei Pengyuan alikuwa afisa mkuu aliyesimamia biashara ya makaa yam awe nchini China.
Mahakama katika mji wa Baoding, kaskazini mwa Uchina, imesema Bw Wei alipokea rushwa alipokuwa akiidhinisha miradi ya makaa yam awe.
Maafisa wa serikali wanasema mashine nne za kuhesabu pesa ziliharibika walipokuwa wanajaribu kuhesabu pesa zilizopatikana nyumbani kwa afisa huyo.
Maelfu ya maafisa wa serikali wameadhibiwa kwenye kampeni kubwa ya kukabiliana na ulaji rushwa nchini China.
Kampeni hiyo ambayo inaungwa mkono na Rais Xi Jinping imepelekea kuadhibishwa kwa baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa Rais Xi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment