AT amesema inatosha sasa watu kumchukulia kama msanii wa Zanzibar. Anataka atambulike kama msanii wa Tanzania, vile vile Diamond au Alikiba hutambulishwa.
Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, AT amewakumbusha mashabiki na wadau wa muziki kuwa hakuna tofauti kati ya msanii anayetokea Njombe, Sumbawanga na Zanzibar kwakuwa wote ni Watanzania. Amedai kuwa wote hao wanatoka mikoa tofauti lakini taifa moja.
Amemtolea mfano Baby J kuwa ni msanii aliyeishi Zanzibar lakini asili yake ni Usukumani na kwamba alienda huko na kuanzia darasa la saba lakini wanajivunia kuwa ni ndugu yao.
“Lakini kwa upande wa bara mpaka leo AT akifanya show anaambiwa kutoka Zanzibar. Lakini wakipanda Weusi ‘aah bwana wanakuja Weusi.’ Hii nayo inaleta matabaka. Huwezi kusema huyu anatoka Zanzibar, huyu hapa anatoka Mwanza, show inafanyika Sumbawanga au inafanyika Njombe. Ni sawa sawa na kusema kuna abiria 10 na mmasai mmoja,” amesisitiza.
Ameeleza kuwa hata suala la tuzo akishinda yeye, watu wataishia kusema ameiapa sifa Zanzibar na si Tanzania.
“Alikiba kwao Kigoma, kwahiyo akishinda tuzo tuseme tuzo kawapa Kigoma,si ni tuzo ya Mtanzania?” amehoji.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment