October 31, 2016

Tokeo la picha la thomas mashali 
 Bondia Thomas Mashali, ameuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira usiku wa kuamkia leo, baada ya kupigiwa kelele za mwizi kufuatia ugomvi uliozuka maeneo ya Kimara, jijini Dar es Salaam.
Bondia, Francis Miyeyusho aliyekuwa mwanafunzi wake, ameiambia East Africa Radio kuwa Mashali aliumizwa vibaya kichwani. Amesema Jumapili hadi saa tisa alasiri walikuwa pamoja kwenye kikao cha masuala ya masumbwi na alimuaga kuwa anaenda Kimara.

“Baadaye nikaja kusikia story kwamba kuna mtu kagombana naye pale wamemchenjia wameanza kumuitia kelele za mwizi mitaa ya Kimara huko kwahiyo wamemchangia raia, wamempiga,” amesimulia Miyeyusho.

Bondia huyo amesema kuwa Mashali alikuwa amenyoa rasta zake na kwamba huenda hiyo ni sababu wananchi wengi walishindwa kumtambua.


Kwa upande wa baba yake mzazi, Mzee Christopher Mashali, amesema alipata taarifa hizo usiku akiwa amelala kutoka kwa vijana wanaomfahamu. Vijana hao walimweleza kuwa mtoto wake amepigwa vibaya kiasi cha kupasuliwa kichwa na usiku huo kuwapigia simu wanae wengine waliopo Dar.

Anasema Mashali alifariki Muhimbili kutokana na kuwa amejeruhiwa mno ikiwa ni pamoja na kutolewa ubongo. Mzee Mashali anasema mara ya mwisho kuwasiliana na mwanae ilikuwa jana (Jumapili) mchana.

“Alinitumia meseji ambayo bado ninayo hapa akaniambia ‘baba nipo kwenye kikao, nikimaliza kikao nitakujibu baba’ ndio mara ya mwisho nimewasiliana naye,” ameeleza mzee huyo.

Amesema kinachoendelea sasa ni kupata ripoti ya polisi, kupewa ruhusa ya kuuchukua mwili wa marehemu tayari kwa mazishi.

Mashali aliyezaliwa mwaka 1980, ameacha watoto watano.

                         

Related Posts:

  • Fid Q, K-sha wapata tuzo zaheshima za EU    Kutoka kulia ni baadhi ya Watanzania waliotunukiwa Tuzo ya Heshima na Umoja wa Ulaya nchini EU, kutokana na mchango wao katika kuliletea taifa maendeleo.   Umoja wa Ulaya nchini umewatunuku tuzo za hes… Read More
  • Twanga Pepeta ndani ya Nyumbani Park Moro Jumapili hii   Hii ni katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mkurugenzi wa Nyumbani Park $ Samaki Spot Morogoro Boss Lady Farida Mees Matlou, utakosaje sasa?? Twanga Pepeta watakupa burudani bandika bandua mpaka kieleweke, njoo… Read More
  • Kenya yapunguza safari zake Tanzania   Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake k… Read More
  • Zitto Kabwe atua rasmi ACT, Apokewa kwa shangwe Zitto Kabwe akionyesha kadi ya uanachama ya Alliance for Change and Transparency (ACT) mara baada ya kukabidhiwa na kujiunga rasmi jana. Akiwa na Kadi namba 007194  Zitto Kabwe akifurahia jambo na mwanachama mwenzake D… Read More
  • Gari la kikosi cha Zimamoto limevunjwa vioo   Picha hii siyo halisi ya tukio   Jeshi la Polisi mjini Tunduma mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliofunga barabara. Akiongea na East Africa Radio kwa njia ya simu Kaman… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE