Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.
Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno
mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja
huyo.
Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.
Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani
mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia
kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii
wake wa WCB, Diamond na Raymond.
Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment