
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfutia shtaka linalomkabili mshtakiwa
Salumu Njwete baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe
mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore amekubaliana na ombi hilo
kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria
ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa
shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa
hukumu.
Mtuhumiwa Salum Njwete maarufu "Scorpion" aliyemtoboa macho Saidi Mrisho alikuwa akikabiliwa na shataka la unyang'anyi.
Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki mshtakiwa huyo endapo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo. #Regrann
Source:Siasahuru.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment