October 16, 2016



Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ameandika haya kupitia ukurasa wake wa facebook



Gavana Benno Ndulu, Mungu anakuona! Ukweli utakuweka huru, hali ya uchumi wa nchi yetu ni mbaya mno. Unapaswa kuwaeleza Watanzania ukweli huo na kushauri njia za kufuata na hatua ambazo serikali inapaswa kufanya. Kuendelea kusisitiza kuwa Uchumi wa nchi unaimarika wakati mambo kibao sana yamesimama serikalini kwa visingizio lukuki ni kujidanganya wewe mwenyewe. Ukweli na Uwazi ni moja ya siri muhimu za Uongozi imara duniani. Niwakumbushe watanzania ule msemo wa Kiganda "...President Museveni has more than 30 Economic advisers, when they convene to advise him it is him (Museveni) who advises the advisers". (Rais Museveni anao washauri wa Uchumi zaidi ya 30, na wanapokaa kumshauri ni yeye "Museveni" ndiye anawashauri hao washauri".

JSM.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE