Klabu ya Azam FC imemtambulisha Adbul Mohammed kuwa General Manager wa
klabu hiyo ambapo mbali na utambulisho huo wameeleza lengo kuu la kumpa
wadhifa huo ndani ya timu yao.
C.E.O wa Azam FC Saad Kawemba amesema lengo la kumwajiri Abdul kama
General Manager ni kuhakikisha mabingwa hao wa kombe la Kagame wanapiga
hatua mbele kwenye upande wa professionalism.
“Tunamtambulisha mwenu Abdul Mohammed, rasmi ni mwanafamilia wa Azam FC,
anaingia moja kwa moja kwenye secretariat ya Azam FC lengo ni
kuhakikisha klabu yetu inapiga hatua kwenda kwenye professionalism,”
amesema Kawemba wakati akimtambulisha Abdul Mohamed.
“Atakuwa ni General Manager wa klabu yetu akishughullika na masuala ya
kila siku yanayohusu klabu yetu. Tunamkaribisha kwetu kwa nia moja
tukiamini uzoefu wake na weledi wake utatusaidia Azam FC kuondoka katika
hatua tuliyopo kwenda hatua nyingine ya mbele zaidi.”
Abdul amesema atahakikisha muundo na muonekano wa Azam unabadilika na kuwa wa kiueledi.
“Nimekuja kwenye klabu ya Azam kwa ajili ya kufanyanao kazi kujaribu
kuona tunaivusha au kubadilisha muonekano na muundo wa klabu kwenda
kwenye hali ya weledi zaidi,” amesema mwandishi huyo wa zamani wa idhaa
ya Kiswahili ya BBC.
“Azam ni klabu changa lakini ni miongoni mwa klabu kubwa Tanzania,
tunataka kuwapa mashabiki wetu aina flani ya utofauti ambao hauwezi
kupatikana kwenye vilabu vingine isipokuwa Azam.”
0 MAONI YAKO:
Post a Comment