Mwenyekiti Mtendaji wa Sahara Media Group, Dr Anthony Diallo
Kampuni kongwe ya habari nchini, Sahara Media Group
itapunguza wafanyakazi wake takriban 100. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa
iliyoitoa kwa wafanyakazi, Jumatatu hii.
Imesema inachukua uamuzi huo kutokana na kuhamisha matangazo yake
kutoka analojia kwenda dijitali na kwamba nia yake ni kupunguza gharama
za uzalishaji. Watakaoathirika ni pamoja na watangazaji, watayarishaji
wa vipindi na wafanyakazi wengine.
Itatumia takriban vinane kupunguza wafanyakazi ikiwemo utendaji,
elimu, umri, nidhamu na vingine na kutumia kipindi cha miezi mitatu
kukamilisha mchakato huo.
Wakati huo huo Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Dr Anthony
Diallo, amekanusha tetesi zilizoenea kuwa kampuni hiyo imenunuliwa na
kampuni ya Nation Media Group baada ya kushindwa kulipa madeni yake.
Madeni hayo ni pamoja na KCB inayodai shilingi bilioni 28, deni la
benki ya Mkombozi, malimbikizo ya mishahara na kodi ya TRA shilingi
bilioni 4.
“Tuna asset net value ya zaidi ya bilioni 110. Tuna mkopo kama
kampuni na benki ya KCB pekee na hatuna deni kama kampuni huko Mkombozi.
Kuuza media company kubwa kama yetu unahitaji kibali cha TCRA,” alijibu
Diallo,.
“Tunapunguza wafanyakazi kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye
automation na kutegemea ununuzi wa vipindi badala ya kuvitengeneza
wenyewe, ubora wa vipindi vya kutengenezwa na wengine ni bora zaidi.”
Hadi sasa kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi zaidi ya 400.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment