Klabu Bingwa ya Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei.
Azam FC tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia marekebisho kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni kukipa nguvu kikosi hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.
Lengo kubwa la Azam FC ni kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu kwa kupata matokeo bora uwanjani, na tunaamini ya kuwa, benchi zuri la ufundi tulilokuwa nalo, wachezaji wazuri walioko kikosini na wengine watakaokuja kuongeza nguvu, wote kwa pamoja wataweza kutuvusha kuelekea safari ya mafanikio msimu huu.
Hivyo, tunawaomba mashabiki wetu kuvuta subira na kuendelea kuisapoti timu kwani tunaamini ya kuwa nyie ndio nguzo muhimu ya 12 uwanjani katika kuwapa hamasa wachezaji ya kupata matokeo bora pamoja na kuijenga timu kiujumla.
Wakati huo huo, tumewapokea wachezaji saba waliokuja kwenye majaribio ya kujiunga na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),
Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.
Imetolewa na Uongozi wa Azam FC
0 MAONI YAKO:
Post a Comment