November 30, 2016

Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

 “Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.

Related Posts:

  • Will Smith kususia tuzo za Oscars                     Will Smith asema anamuunga mkono mkewe Jada Pinkett smith kususia onyesho la tuzo la Oscars 2016 Msanii… Read More
  • Darassa amekuletea hii mpya Mkali wa Hip Hop toka Tanzania Darassa, amekuja tena na wimbo wake huu mpya unaitwa kama Utanipenda. Darassa katika wimbo wake huu mpya amekuja na mwanamuziki mkali katikam anga ya bongo fleva bwana Rich Mavoco … Read More
  • Uchaguzi Zanzibar,i ZEC wataja Tarehe Tume ya Uchaguzi ya zanzibar ZEC imetangaza tarehe rasmi ya kurudiwa kwa uchaguzi  mkuu visiwani humo kuwa ni  2o March 2016 Taarifa hiyo imetolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeb… Read More
  • Bunge limemuangusha Rais Magufuli - Mtatiro   Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanasheria kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro amesema Bunge limemwangusha Rais Magufuli kwa kuchagua kamati dhaifu katika kamati zilizotangazwa hivi karibuni. Akiel… Read More
  • Tokomeza kipindupindu yazua tafrani Morogoro Mgambo wa Manispaa ya Morogoro wakiwakamata kwa nguvu baadhi ya Wananchi waliokaidi zoezi la kuondolewa kwa mama ntilie katikati ya Mji   Mgambo wa Manispaa ya Morogoro wakishirikiana na Jeshi la Polisi pa… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE