
Zena Mswagala
Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Morogoro Mjini, imetoa tamko lake juu ya msimamo wa Baraza kuu la uongozi CU taifa. Wakitoa tamko hilo kwa wana habari leo hii 13 November CUF Morogoro wamesema wamelaani hatua iliyofanywa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa Prof. Ibrahim Lipumba kwa kitendo chake cha kuvamia ofisi za chama na kufanya uharibifu wa lasilimali za chama
Taarifa hiyo ya CUIF Morogoro inasomeka:
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF –Chama Cha Wananchi)
P.O.BOX 670
Morogoro Mjini
Simu: 0715 282331
0785 397107
TAMKO LA VIONGOZI WA JUMUIYA ZA CHAMA MOROGORO MJINI KUHUSU KUUNGA MKONO MAAMUZI YA
BARAZA KUU LA UONGOZI TAIFA
Imetolewa na;
Viongozi wa wilaya Morogoro Mjini
Leo tarehe 13/11/2016
Ndugu wanahabari,
Awali hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujaalia afya njema na kukutana leo pamoja nanyi ili tuweze kuelezea msimamo wetu juu ya hali ya kisiasa inayoendelea ndani ya chama chetu na kwa kupitia kwenu watanzania waweze kupata taarifa hii na msimamo wetu.
Sisi viongozi wa Jumuiya za chama cha wananchi CUF wilaya Morogoro Mjini tumekutana tarehe 13 Novemba, 2016 kujadili suala linaloendelea hivi sasa ndani ya chama chetu kwa aliyekuwa mwenyekiti wetu Taifa Prof Ibrahim Lipumba akisaidiwa na msajili wa vyama vya siasa nchini kutaka kulazimisha kurejea katika nafasi ya uenyekiti ambao yeye mwenyewe kwa utashi wake aliamua kujiuzuru mwaka jana tarehe 5/8/2015. Chama kupitia bodi ya wadhamini wamelichukulia suala hili kwa njia za kisheria na kufungua shauri la madai namba 23/2016.
Baada ya kutafakari kwa kina suala hili kupitia vikao vya Jumuiya ya Vijana na Wanawake kwa pamoja tumekubaliana kutoa msimamo juu ya suala hili kama ifuatavyo:
1. Tunalaani vikali hatua ya Ibrahimu Lipumba kuvamia ofisi ya chama chetu Buguruni na kufanya uharibifu wa mali za chama na kusababisha hasara kwa chama na kuwajeruhi walinzi waliokuwepo katika zamu siku hiyo. kitendo hicho kimeiharibia chama taswira yake njema mbele ya jamii na kukivunjia heshima chama chetu na yeye binafsi.
2. Tunalaani kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuingilia suala hili kinyume na majukumu yake yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa (Political Parties Act, 2008) hali akijua wazi kuwa hana mamlaka kisheria kufanya hivyo alivyofanya kwa lengo la kutaka kukiyumbisha chama chetu kwa maslahi ya ofisi yake na wanaomtumia.
3. Tunatoa pongezi kwa viongozi wa chama Taifa kwa kuendelea na msimamo usiyoyumba wa kusimamia maslahi mapana ya chama, na kukataa kabisa kuruhusu vibaraka wa CCM kuingia ndani ya chama na kutaka kurudisha nyuma juhudi za mapambano ya kisiasa kuing’oa CCM madarakani mwaka 2020. Sisi viongozi na wanachama wa CUF kutoka wilaya ya Morogoro Mjini tunaunga mkono maamuzi sahihi ya Baraza Kuu la Uongozi Taifa yaliyofanyika tarehe 27/9/2016 ya kuwachukulia hatua za kinidhamu Ibrahimu Lipumba na wenzake ambao wameoneka kukiuka katiba ya chama na taratibu za uongozi wa taasisi yetu huku wakiwa na nia ya kudhoofisha harakati za kudai Haki, Usawa Na Mabadiliko Ya Kisiasa Na Kiuchumi katika nchi yetu.
4. Tunalipongeza jopo la wanasheria wa Chama na wadau wengine ambao wamekuwa wakifanyakazi kubwa ya kushirikiana na Chama kuhakikisha hatua sahihi za kisheria zinachukuliwa kwa uharaka dhidi ya wale wote wanaokusudia kukihujumu Chama. Tunaiomba mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaamu kulisikiliza shauri hili kwa uharaka na kusimamia haki bila upendeleo.
5. Tumepokea kwa furaha na hamasa kubwa mipango ya chama iliyoandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa na kutolewa hivi karibu ikiwemo kufanya ziara nchi nzima, maandalizi na mipango mkakati ya kuelekea mwaka 2020 pamoja na kuendeleza mashirikiano ya UKAWA ili kujenga nguvu ya pamoja kuishinda CCM mwaka 2019/2020 kwa angalizo la kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza wakati uliyopita.
Ndugu wanahabari;
Tunapenda kutoa wito kwa wanachama wa CUF na watanzania wote wapenda mabadiliko;
Katika kuweka mkazo wa Tamko hili KATIBU WA JUMUIYA YA VIJANA WA CUF-JUVICUF Morogoro Mjini Mheshimiwa Dotto Malenda amesema;
“Vijana wanatambua na kukubaliana na maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa. Prof Lipumba aliondoka katika kipindi kigumu na muhimu kisiasa kwa kudai nafsi yake imemsuta, je kurudi kwake Nafsi haimsuti tena? Vijana wa Morogoro wanaungana na viongozi na wanachama wa wilaya nyingine Tanzania kusimamia maamuzi ya chama. Vijana wanataka UKAWA uendelee kwa kuboresha na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. UKAWA ndio Mpango mzima kuweza ‘kudeal’ na CCM. Uwezi kulazimisha jambo kwa gharama kubwa wakati ulipata ridhaa ya wanaCUF bila gharama wakati huo. Mpango wa kuvuruga chama pale Ubungo Plaza ulifeli. Sasa ametumwa kuja kuvuruga tena. Chama kimepata mafanikio makubwa katika kipindi ambacho yeye alijitenga nacho. Mlango wa kurudi kwake umeshafungwa na maamuzi ya vikao vya juu. Majira ya kisiasa yamemuangukia kama alivyosema marehemu muasisi wa chama Shabani Khamisi Mloo. Hana nafasi tena ndani ya CUF. Tunamtaka prof Lipumba ajiheshimu na kuacha kushirikiana na wahuni kufanya vitendo vya kihalifu na kuyumbisha chama chetu cha CUF. Wasaliti wa Chama Morogoro tunawajua na hawakuanza leo, walishiriki kutaka kuwarubuni wagombea Ubunge wa mikoa ya kusini ili wanunuliwe na CCM waachie majimbo yao ambayo leo ndio yamekiletea ushindi chama. Wanachama waliokuwa hawafahamu mpango huu warejee kundini na kuungana na wanaNGANGARI wenzao na kuachana na wavuruga chama wahafidhina.”
HAKI SAWA KWA WOTE
______________________
ZENA MSWAGALA
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WANAWAKE JUKECUF-MOROGORO MJINI
______________________
JUMA MUDHIHIRI
MKURUGENZI WA HABARI NA SERA JUVICUF-MOROGORO MJINI
0 MAONI YAKO:
Post a Comment