
Katika Gaazeti la Mwananchi la leo 18 November 2016, katika ukurasa wake wa Mbele, kuna maswali matano yaliyomlenga Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh: Poul Makonda yenye kichwa cha habari kisemacho "Kauli za Makonda zaibua maswali 5" Clouds Fm haikukaa kimya ikamtafuta Mh: Makonda kujibu maswali hayo yaliyochapishwa na Mwananchi.
Maswali yalikuwa haya:
1. Kwanini Makonda hukuchukua hatua dhidi ya hao watu 10 wanaomueleza wanataka kumpa 50Million Kila Mwezi ili kumyamazisha?
2.Kwanini hakutaja majina yao kwa Vyombo husika ili vifanye uchunguzi na Kuchukua hatua?
3. Alipoambiwa kuwa waziri mkuu karuhusu Shisha kwanini hakwenda kumuuliza hadi akayasema hadharani?
4. Kamanda Siro na Kaganda ni wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwanini hakuwapa maelekezo huko na kwenda kuwachongea kwa waziri mkuu?
5. Hayo yote yanaibua Swali la Mwisho Kulikua na Ulazima gani wa kutoa tuhuma hadharani kwa viongozi hao wakati serikali Ina mfumo wake wa mawasiliano na vyombo ya Uchunguzi?
Majibu ya MH: Makonda
Makonda amesema waandishi wahangaike kuelimisha kuhusu madhara ya shisha na sio kuhangaika na kauli ambayo haina madhara.
Pia amesema kutamka hadharani ni kuongeza awareness.
Pia amesema hakutaja majina kwa kuwa majina hayatajwi hadharani.
Maana ya kumuuliza waziri mkuu hadharani ni ili umma upate majibu, akiuliza kwa kificho wengine wanaweza wasiamini majibu au wasiyapate.
Makonda amedai ameshuhudia shisha inauzwa maeneo hadharani kabisa na kuuliza polisi wanasema hakuna.
Makonda amesema wanafanya kazi kwa uwazi kwa hiyo hakuna haja ya kuficha ficha na kuulizana sirini
0 MAONI YAKO:
Post a Comment