Msanii wa Nigeria anayetarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta
Jumamosi hii ya Novemba 5, Yemi Alade amemsifia Nandy kwa kudai kuwa
alitabiri atakuwa msanii mkubwa.
Nandy ni msanii mmoja wapo aliyechaguliwa kuwasha moto kwenye tamasha hilo, wasanii wengine ni pamoja na Weusi, Maua Sama, Navy Kenzo, Alikiba, Mr Blue, Rayvanny, Darassa, Jay Moe, Barakah The Prince, Bill Nas, Fid Q, Belle 9 na wengine.
Tekno, Yemi Alade na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Fleva wakiongea na waandishi wa habari
Wasanii wengine kutoka nje ya Tanzania ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo ni pamoja na Tekno (Nigeria) na Chameleon (Uganda).
0 MAONI YAKO:
Post a Comment