Producer maarufu wa THT,
Emmanuel Maungu ‘Emma The Boy’ amepata ajali mbaya ya gari hivi punde
maeneo ya Kabuku karibu na Segera, Tanga wakati akitokea Dar es Salaam
kuelekea nyumbani kwao, mkoani Tanga.
Imeelezwa kuwa, Emma ameumia zaidi maeneo ya kifuani na shingoni na kilichomsaidia asiumie zaidi, alikuwa amefunga mkanda.
Akizungumza moja kwa moja na mwanahabari
wetu, kaka wa Emma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa,
kwa sasa mdogo wake huyo amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tanga
akipatiwa matibabu kutokana na maumivu na majeraha makubwa aliyoyapata.
“Ni kweli Emma amepata ajali mbaya
sana wakati akitoka Dar kwenda nyumbani Tanga, ameumia kifua na shingo
na maeneo mengine, gari alilokuwa akisafiria limeharibika vibaya sana,
tumuombee kwa Mungu aweze kupona,” alisema.
Aidha haijaelezwa chanzo cha ajali hiyo ni nini.
Msanii mwingine kutoka THT, Hamadai
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Emma The Boy ametengeneza nyimbo
karibu zote za msanii Barnaba na wasanii wengine wa THT.
Taarifa zaidi za tukio hilo tutazitoa kadiri tutakavyozipata.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment