December 02, 2016




Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mzee Yusufu  Makamba asema Rais Magufuli anafanana na Yohana Mbatizaji kwa vile ni kiongozi  anayefanyakazi bila kuogopa.

Makamba ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu katika mahojiano maalum na  Mwandishi  wa habari hizi. Alisema kuwa  Rais ni kiongozi mchapakazi ambaye hayumbushwi na maneno wala vitisho  kwa vile anasema ukweli katika kutekeleza majukumu yake.

“Yohana Mbatizaji alisema ukweli na hakutikiswa na upepo, hakuogopa macho ya watu wala hakuwa mtu wa majigambo, kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu Marko 6:12, na hivyo ndiyo navyomfananisha Rais wetu Magufuli na viongozi wote tumuunge mkono” alisema Makamba.

Aidha, kuhusu miaka 55 ya Uhuru , alisema kuwa ni vyema Watanzania  wakazingatia wito wa uhuru ni kazi, na kwa kuwa Serikali hii imeweka mkazo katika ufanyaji kazi.

Makamba  alisema kuwa katika Awamu hii ya HAPAKAZI TU, inaakisi wito wa Uhuru katika vipindi mbalimbali kuanzia kipindi cha Uhuru ni kazi na Uhuru na kazi mara baada ya kupatikana kwa Uhuru  na kuwakumbusha  watanzania kuulinda Uhuru.

“Ni lazima kuulinda Uhuru kwa gharama yeyote ili amani na mshikamano uendelee kuwepo basi hatuna budii kuepuka lugha zenye  maneno ya uchochezi, ukabila na udini” alisema Makamba

Related Posts:

  • New Audio: Koba - Zawadi Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye mkongwe wa muziki wa Bongo fleva MC KOba au Koba, amekuletea wimbo wake mpya kabisa, unaitwa zawadi ameimbakatika maadhi ya Mchiriku au Mnanda.  Download hapa chini … Read More
  • New Audio: Mzalendo - Suma G   Huyu jamaa ni kutoka Hot Pot Family, kitambo sana alipote. Ni mzee wa Usawhili Suma G, anakualika kusikilza wimbo wake mpya uitwao mzalendo.  Download hapa chini … Read More
  • Kala Pina kugombea udiwani kwa ACTMsanii wa muziki  wa Rap toka Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud aka Kalapina (kushoto) akipokea fomu za kugombea udiwani kata ya Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo toka kwa msimamizi msaidizi … Read More
  • Lowassa, Arusha ni gharika, waziri Marsha ajiunga CHADEMA 1.Lawrence Masha akabidhiwa kadi na Mbowe (waziri w zamani wa mambo ya ndani) 2.Daniel Porokwa - katibu wa ccm Manyara 3.Robinson Mwenyekiti wa uv ccm Arusha 4.Sioi Sumari (huyu alikuwa mshindani wa Joshua Nassari Arumeru Ma… Read More
  • Mbio za urais 2015. Lowassa afunika Mbeya leo Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ukawa baada ya kutua Jijini Mbeya leo kwa lengo la kujitambulisha .. Kikosi kazi kikiwata… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE