Aliyekuwa mwanachama mstari wa mbele na mgombe ubunge jimbo la Morogoro mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo 2015 Selemani Abdallah Msindi "Afande Sele" amejiondoa uanachama wa chama cha ACT wazalendo na kukaa mbali na siasa. Katika ukurasa wake wa Facebook na kuthibitisha kupitia ubalozini.blogspot.com afand ealiandika
"Habari za wkt huu akina ndugu nyote,naamini tupo pamoja ktk kujitafutia maisha na kulijenga taifa letu pendwa Tz ambalo ndani ya katiba yake kuna kipengele muhimu kinachotupa UHURU kwa kila mtu kufanya mambo yake apendavyo ilimradi tu havunji sheria za nchi....sasa kwa kuzingatia UHURU huo tuliopewa na KATIBA yetu mimi Leo natangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT-Wazalendo na kutokua mfuwasi wa chama chochote cha Siasa bali nitabaki kuwa raia wa kawaida ndani ya nchi yetu huku nikiendelea na majukumu yangu mengine ya kimaisha mpaka hapo nitakavyoamua vingine kama nitakua na sababu ya kufanya hivyo...Nawatakia kila la kheri wote waliobaki ndani ya chama pia nawatia moyo mkuu wa kuendeleza harakati za ujenzi wa chama ili kuleta upinzani sahihi na imara utakaosaidia kujenga taifa kwa faida yetu na vizazi vijavyo...naomba ieleweke kuwa uamuzi huu'tarajiwa'sijauchukua kwa bahati mbaya hivyo naomba kila mmoja awe wa ndani au wa nje ya chama chetu aheshimu uamuzi wangu kama mimi ninavyoheshimu maamuzi ya watu wengine kwa mujibu wa KATIBA ya nchi inavyosema...Ahsanteni sana wadau tukutane MAISHANI...
Baada ya kuansdka hivyo, Machaku Media ilimtafuta afande sele na kuthibitisha kuondoka kwake ndani ya chama hicho akida, umwinyi wa viongozi wa chama hicho, kutaka kusikilizwa wao, kukataa ushauri ndicho kilichomfanya Afande Sele kujiondoa na kuwaachia chama chama chao. "Ni kweli nimeandika kujiondoa uanachama kwa hiari yangu bila kushawishiwa, Nimefanya kama walivyofanya kina Mwigamba, Mchange na kina mkosa mali, chama hakina dila, chama kimeshikwa na wachache wenye chama chao, hawashauriki, wao ni wao, tukiwaambia kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu hawataki, hatuwaelewi mambo yao, nimeamua kujiondoa kufanya mambo yangu mengine" amemaliza Afande Sele
0 MAONI YAKO:
Post a Comment