Bifu jipya limeibuka katika muziki wa kizazi kipya mkoani Morogoro baada ya Mtayarishaji wa muziki mkoani hapa kutoka studio za kwanza Records Vent Skillz kuamua kusitisha kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Hip Hop Meddy Botion pamoja na Mash J mbao ni vizazi vya Super Nyota mkoani Morogoro waliokuwa katika label ya MokoMoko Movement.
Vennt Skillz producer toka kwanza Records inayosimamia Mokomoko Movemennt
Akizungumza katika Interview kwenye show ya Gwaride kupitia Abood Fm pamoja na mtangazaji Abe Kidunda, Mtayarishaji huyo ametaja sababu kubwa iliyofanya uongozi wa label hiyo kuamua kukacha kufanya kazi na wasanii hao ni kuingiza kazi na mapenzi ambapo inadaiwa wasanii hao walikuwa wakimgombania moja ya wasanii katika studio hiyo aliyetambulika kwa jina la Jamila.
Aidha wakati mtayarishaji huyo akiendelea kutoa ushahidi kuhusu sababu iliyopelekea kusitishwa kwa wasanii hao kufanya kazi katika studio hiyo, ikabainika baadhi ya picha zilizopo katika account ya Instagram ya msichana Jamila kuwa tayari yupo na ujauzito wa Meddy Botion na mwezi wa sita anataraji kujifungua. Meddy Botion alikuwa mshindi wa kwanza katika shindano la Super Nyota mkoani Mprogoro mwaka 2016 na mshindi wa tatu kitaifa akitamba kwa sasa na single yake inaitwa Sura huku Mash J akiwa tayari ni msanii aliyewahi kutamba na kazi nzuri za muziki wa hip hop ikiwemo Mpera Mpera aliyomshirikisha Stamina na Taarifa aliyomshirikisha G Nako.
Medy Botion
Mtayarishaji huyo alifunguka kuwa baada ya kuachana na wasanii hao nguvu zake sasa anazielekeza kwa msanii Rota ambaye kwa siku za usoni ndiye atakayekuwa chini yake huku akiweka wazi mwaka 2017 mwanzoni wanataraji kuachia kazi mpya. Rota Msanii mpya chini ya Producer Vent Skillz Zaidi Sikiliza hapa Interview hiyo unaweza pia kuipakua bure kabisa
Lotta Komba msanii mpya chini ya Mokomoko Movement
0 MAONI YAKO:
Post a Comment