Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura mapema leo 20 Desemba 2016 amezindua mpango maalum wa mchango wa Sanaa Kiuchimi unaotarajiwa kuongezeka kupitia mauzo ya kieletroniki mtandaoni ambapo itapelekea upatikanaji wa Haki na maslahi ya Wasanii wenye vipaji bunifu mpangp huo ujulikanao kama ‘Creative Talent Management Programme, CTMP).
Naibu Waziri Mh. Anastazia Wambura akizungumza katika tukio hilo, ametoa wito kwa watanzania wenye vipaji na uwezo katika masuala ya sanaa kujitokeza na kuanzisha mipango yenye nia thabiti ya kukuza sanaa na utamaduni hapa nchini kwani wajitokezapo inasaidia kutambulisha Sanaa ya nchi.
“Tanzania inakadiliwa kuwa na zaidi ya Wasanii Milioni 6. Mtu yeyote mwenye uwezo na kipaji ajitokeze kuwasilisha mawazo yake ambayo yatasaidia kuinua sanaa yetu hapa nchini. Usiogope kurogwa maana wengi wanakuwa na mawazo mazuri lakini wanashindwa kujitokeza kwa kuhofia uchawi, kwani uchawi ni utamaduni usio shikika, tujitokeze kwa wingi katika kuonyesha uwezo wetu” amesema Mh. Wambura akitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kuandaa mipango mbalimbali ya kusaidia sanaa na utamaduni wa watanzania.
Pia aliwaomba wasanii kuhakikisha wanatambulika kwa uwezo wao ikiwemo kuwa na hakimiliki kutoka COSOTA, BASATA na mamlaka zingine mbalimbali ili kazi zao ziwe katika usalama.
Kwa upande wake, Rais wa TCDB ambao ndio waandaaji wa mpangop huo, Mwalimu Carolus Bujimu amesema kuwa, mpango huo ni matokeo ya utafiti uliobaini uwepo wa wasanii wengi wenye vipaji katika Nyanja mbalimbali za sanaa huku wakikabiliwa na changamoto za kiuchumi na kukosa ubunifu.
“Baada ya kubaini ili, CTMP itakuwa mchango tosha kuinua wasanii wa Tanzania, kwani watapata kuhifadhiwa kazi zao na kuwa na hakimiliki pamoja na kupata soko la uhakika. Pia tutakuwa na nafasi ya kipekee katika kuuza kazi za wasanii kupitia njia ya mtandao yaani ‘Online’ na pia kazi zao zitauzwa Tanzania nzima kuanzia ngazi ya kijiji, mji, mijii mpaka majiji kwani kwa kushirikiana na shirika la Posta hapa nchini watafikia malengo yao hayo. Alieleza Mwalimu Carolus.
Aidha, mpangp huo wa CTMP umeweza kuwashirikisha wadau muhimu wakiwemo TRA, TCRA,Jeshi la Polisi, Shirika la Posta, GS1 (t)Ltd,TBC,Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBa),BASATA,COSOTA, Shirika la Muziki Tanzania, Mwalimu Nyerere Foundation na wengie wengi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipokelewa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya. kuliani anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi. Wakati Waziri akiwasili kwenye tukio hilo la uzinduzi wa mpango wa CTMP, mapema leo 20 Desemba 2016
Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi akimkaribisha Naibu Waziri Mh. Anastazia Wambura wakati wa tukio hilo la uzinduzi wa mpango wa CTMP, mapema leo 20 Desemba 2016.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment