Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema kuanzia mwakani wizara yake itaanzisha tuzo mahsusi kwaajili ya blog za Tanzania.
Akizungumza wakati akifunga mkutano mkuu na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini, TBN jijini Dar es Salaam Jumanne hii, Nape amesema kwa kazi kubwa ambayo blog zimekuwa zikiifanya katika kuhabarisha umma, ni muda wa kuanza kuwatuza wale wanaofanya vizuri.
Amesema alipata wazo la kuja na tuzo za aina hiyo wakati akisafiri kwenye ndege na kuona jarida linaloelezea tuzo za blog za Kenya na kuona kuwa kuna ulazima wa Tanzania pia kuwa na tuzo hizo.
Nape amedai kuwa lengo la tuzo hizo zitakazotolewa mwanzoni mwa mwaka ujao, zitakuwa ni kwaajili ya kuzisaidia blog kuweza kuwa na ‘specialization’ katika maudhui mbalimbali.
Amesema tayari ameshaanza kuzungumza na makampuni na taasisi mbalimbali kwaajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapewa zawadi kubwa ili kuwahamasisha zaidi. Ameahidi kuwa tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi na kwamba makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini
0 MAONI YAKO:
Post a Comment