Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba.
Kufuatia kifo cha mama mjamzito katika duka la dawa mkoani Singida, Jeshi la Polisi mkoani humo linawashikilia watu wawili, akiwemo mmiliki wa duka la dawa muhimu za binadamu katika kijiji cha Itagata wilayani Manyoni, kwa tuhuma za uzembe wa kusababisha kifo cha mjamzito huyo, Heleni Maduhu (29).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mume wa marehemu, Bahame Kamuda (32) na Joseph Hengwe (50) ambaye ni mmliki wa duka la dawa katika kitongoji cha Kilulumo, kijiji cha Itagata Tarafa ya Itigi wilayani Manyoni.
Kamanda huyo alidai kuwa wakiwa njiani, mumewe aliona hali ya mkewe inazidi kuwa mbaya zaidi, aliamua kumpeleka kwenye duka la dawa muhimu linalomilikiwa na Hengwe lililopo jirani ambapo alijifungua mtoto wa kiume.
“Kutokana na mjamzito huyo kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua, mumewe aliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Misheni ya Itigi kwa pikipiki lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kufika mbali kabla ya mama huyo kufariki dunia,” alisema Magiligimba.
Kamanda Magilimba alisema tukio lilitokea kitongoji cha Lulanga kijijini hapo Januari 25, mwaka huu saa 9.30 alasiri.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment