Kundi la muziki wa kizazi kipya mkoani Morogoro la Mokomoko Movement, limemalizana tofauti zao na sasa kufanya kazi pamoja kama zamani. Wakizungumza na waandishi wa Habari mjini hapa, wasanii hao wamesema wamemalizana tofauti zao zilizowaweka kando kwa muda. Producer toka kwanza Records Vennt Skillz ambaye ndiye kiongozi wa kundi hilo, alitangaza kuwastopisha kufanya kazi na Wanaii Mash J na Medy Botion kutokana na ugomvi wa kimapenzi uliozua gumzo mkoani hapa. Wasanii Medy Botion na Mash J ambao ni washindi wa Super Nyota miaka tofauti, Mash akiwa 2012 na Medy ni Mshindi wa super Nyota 2016 na ndiyo mshindi namba 3 wa kitaifa, wamefurahi baada ya kumalizana tofauti hizo na kuahidi kwamba watakuwa bega kwa mega na mtayarishaji huyo na kwa maslahi ya sanaaa ya Morogoro.
Kwea upande wake mtayarishaji wa Video toka Morogoro G Q, amewaadi wasanii hao, kama kweli wamemalizana tofauti zao , amesema yupo tayari kuwapa ofa ya vide ya kazi zao kuanzia siku ya jana . Baadhi ya wadau wa muziki na wana habari mkani hapa, wamelisifu jambo hilo kuwa ni la kikomavu kisanaa na kwa sasa wasanii hao wamekuwa na kujitambua nini wanafanya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment