February 22, 2017

Watu watatu wameuawa katika tukio la kiuhalifu akiwamo mkuu wa upelelezi wilaya kibiti mkoani Pwani


Tukio hilo lilitokea jana saa moja usiku  katika kizuizi cha kutoza ushuru wa mazao ya misitu eneo la Jaribu Mpakani wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambapo watu wanne wenye silaha walivamia katika kituo hicho na kuwaua wafanyakazi wawili ambao ni  Rashid Mgamba, mlinzi wa kituo hicho,  na Afisa uvuvi Peter James .
Watu hao pia walimuua kwa kumpiga risasi tumboni mkuu wa upelelezi wilaya ya Kibiti ASP Peter Kubezya , ambaye alikuwa amefika kusaidia akiwa katika opereshen maalumu.
Mara baada ya tukio hilo watu hao  walikimbia na kutelekeza piki piki zao mbili pia  waliacha kipeperushi kinachosomeka kuwa  kupinga uwepo wa kizuizi cha kutoza mazao ya misitu ikiwemo mkaa kwani walidai ni kudhulumu wananchi wabeba mkaa

                                                                          

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE